Kidokezo vya kusoma kwa wazazi

Kuwasomea watoto hata kabla hawajaweza kusoma wenyewe-ni ufunguo wa mtoto wako kufanikiwa shuleni baadae!

kuwasomea watoto hujenga lugha na ujuzi wa kusikiliza,hujenga ubunifu,na kuwafundisha kufurahia kusoma na kujifunza mapema.

Unaweza ukachagua vitabu vyovyote ndani BookSmart kusoma na mtoto wako.Ili huu mwongozo utakupa majibu kwa baadhi ya maswali ya kawaida,kuhusu namna ya kuanza:

Nini nisome?

Mtoto anavutiwa na nini zaidi? Je anapenda wnayama? Herufi? Nyimbo na mfuatano wa mwendo? Anza na kitu mtoto anapenda …amini usiamini,kwa watot wadogo kitabu kinapokuwa cha kufurahisha zaidi,kinakuwa cha manufaa zaidi kwa mtoto wako!Na kama hauna uhakika mtoto wako anapenda kusoma nini,muulize!

wapi nisome?

Mtoto nyumbani kwako,shuleni au sehemu ingine yoyote hapo katikati.Kaaa karibu na yeye au muweke kukaa mapajani mwako.

lini na mara ngapi?

Wakati wowote ni muda muzuri wa kusoma na mtoto!Ingawa wazazi wengi na watoto hufurahia kusoma pamoja kabala watoto hawajaenda kulala usiku.

Kwa muda gani??

Tunapendekeza kutumia dakika 10 kila siku kumsomea mtoto wako.Kusoma mara kwa mara ni ufunguo!

gani nasoma?

Ilimradi unaposoma Vitabu mtoto wako anapenda mara kwa mara,huwezi kukosea! Baadhi ya vidokezo hivi hapa…

Chukua muda kuuiza maswali mara kwa mara kuhusu hadithi.Hii inaweza ikawa…

…Maswali kusaidia mtoto kujihusisha na hadithi,kama "Ungejisikiaje kama hichi kingekutokea wewe?"

…Maswali kuhusu kile kinachoweza kutokea au kutotokea kwenye hadithi hiyo,kama "Unadhani nini kitatokea baadae?"

…au onyesha ,jina na taarifa zaidi za picha kwenye hadithi.Kwa mfano ,kama kuna picha ya Tembo kwenye hadithi,unaweza ukauuliza,"jina la huyu mnyama ni lipi? Yeye hupiga kelele gani?"

Na kama mtoto akikuuliza umsomee tena hadithi …fanya hivyo!Kurudia hadithi husaidia watoto kujifunza zaidi na kufikiri kuhusu hadithi.Wanaweza wakasoma na wewe bora zaidi wakishajua hadithi.

bado huna uhakika pakuanzia?

Hivi ni Baadhi ya Vitabu unavyoweza kuanza navyo:

US